3 Aprili 2025 - 01:26
Kijana wa Lebanon ambaye alinadi akiwa karibu na Al-Kaaba (kwa kupaza sauti ya wito) wa "Mahdi aliyeahidiwa", ameachiwa kutoka katika jela ya Saudia

Kijana wa Lebanon, ambaye alinadi kwa sauti akitoa wito /shiari ya "Mahdi Aliyeahidiwa" pindi alipokuwa karibu na al-Kaaba, ameachiliwa baada ya miaka mitatu ya kuwa mateka katika jela ya Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Kimataifa la Ahl al-Bayt (a.s) - Abna - "Haider Salim", kijana wa Lebanon ambaye (alinadi) alitoa shiari ya "Mahdi Aliyeahidiwa" -Labbaika ya Mahdi - pindi alipokuwa karibu na Al-Kaaba, aliachiwa huru baada ya kifungo cha miaka mitatu katika jela ya Saudia na kurejea Lebanon.

Kwa wakati huo, akiwa kando ya Al-Kaaba alinadi na kusema kwamba siku moja Mahdi wetu atakuja na atasema, Mimi ni Imam Mahdi, Mimi ni Imamu Qaim, Mimi ni Imam wa kulipiza kisasi.

Your Comment

You are replying to: .
captcha